Akizungumza na waandishi wa habari katika ghala la Dar es Salaam Inland Container Depot (DIC) leo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya udalali ya Yono (Auction Mart), Scholastica Kevela alisema wataendelea na mnada hadi makontena hayo yauzike.
“Mnada umekuwa ‘very successful’ tumeuza mali za aina tofauti tofauti yakiwamo magari na bidhaa nyinginezo. Mnaniuliza makontena mangapi, mimi kwa upande wangu nimeuza kama nilivyopewa maelekezo,” alisema na kuongeza “Makontena yalikuwa 20 bei imefika hapo ilipofika na tunaendelea na marketing. Kama ilivyosema serikali kwamba huu sio mwisho wa Mnada, kwa hiyo tutaendelea mpaka makontena yote yapate wateja.”

